MAOMBI YA UZAO WA TUMBO
fasting
yearly

MAOMBI YA UZAO WA TUMBO

Monday, June 1, 2026
07:00 PM
Online

Official Event Broadcast

About the Event

Tutakuwa na maombi ya kufunga kwa siku tatu kuanzia tarehe 1 mpaka 3 mwezi wa 6 mwaka huu. Tutafunga kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 12 jioni na kila siku jioni tutakuwa live katika channel yetu ya YouTube tukiomba pamoja kuanzia saa nne kamili usiku mpaka saa tano na nusu usiku. Na kila siku nitakuwa ninatoa muongozo wa maombi. Na wewe utaandika mahitaji yako ambayo unahitaji Mungu akutendee yakiwa na mistari ya kusimamia.

Maombi haya ni kwa ajili ya uzao wa tumbo. Tutaomba na watu wote lakini ni maalumu zaidi kwa wale wanaotafuta watoto, wenye shida za uzazi wanaume kwa wanawake, wenye magonjwa ya tumbo, wajawazito, mabinti ambao hawajaolewa bado, wazazi wanaohitaji Bwana aguse uzao wa tumbo, una hitaji kuombea watoto wako n.k kwa hiyo yatakuwa maombi ambayo tutaombea maeneo mbalimbali.

Wenye matatizo ya kiafya au wajawazito au wanaonyonyesha wanaweza kufanya maombi haya wakiwa wanakula au kuacha baadhi ya vyakula au vitu visivyo vya muhimu ambavyo vina wanakuchukulia muda na muda huo wakautumia katika maombi na kusoma neno.

Jitahidi usikose maombi haya. Pia mwalike na mwenzako. Hata kama hapitii kwenye changamoto hizo au hata kama hatafunga ni vizuri kumwalika tu katika maombi haya tukaomba pamoja. Hakika atarudi na ushuhuda.

Kwa hiyo usikose, ni siku tatu za baraka za kumuona Bwana akitenda katika maisha yetu.

MSTARI TUTAKAOTEMBEA NAO KATIKA MAOMBI HAYA NI:

"Kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu."
Luka 1:37

Ubarikiwe sana.

Innocent Morris
+255652796450 (WhatsApp)

Public Entry
Open Invitation

No RSVP is required for this event. All members, visitors, and searchers are warmly welcomed to attend.

Send Inquiry

Join the Community