KWA MUNGU KUNA MAJIBU YOTE
Teaching

KWA MUNGU KUNA MAJIBU YOTE

Innocent Morris
September 15, 2026
1 min read

Hakika kwa Mungu kuna majibu yote. Ukisoma Biblia yako vizuri, utaona watu mbalimbali waliokuwa na shida mbalimbali walikwenda kwa Mungu na kuomba na wakapata majibu ya maombi yao.

Tunaona Paulo na Sauli walipokuwa wamefungwa gerezani, walipoomba, Mungu alijibu na milango ya gereza ikafunguka.

Ayubu alipokuwa anapitia katika majaribu mazito na magumu, aliomba na Mungu akasikia, na kumvusha katika majaribu yake.

Hezekia alipokuwa katika hali ya kufa alimlilia Mungu, naye Mungu akamsikia na kumvusha katika majaribu hayo.

Mama aliyekuwa anatoka damu kwa miaka 12, alipoamua kwa imani kugusa pindo la Yesu, alipokea uponyaji wake. Haleluya.

Kwa Mungu kuna majibu yote, jambo lolote gumu ulilokosa jibu, Mwambie Yesu naye atatenda.

"Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana."
Mathayo 19:26

Ubarikiwe sana.

Reference Scriptures

01

Mathayo 19:26

Share This Teaching