INSI YA KUMTAFUTA MUNGU KATIKA KUFUNGA NA KUOMBA
Biblia inasema
"Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote."
Yeremia 29:13
Mpendwa, kufunga siyo tu kuacha kula au kunywa kwa muda fulani, bali kufunga ni kujitenga kwa kusudi la kumtafuta Mungu kwa moyo wote. Tunapofunga, tunaacha baadhi ya mambo yanayotushughulisha ili tupate muda zaidi wa kumtafuta Mungu, kusoma Neno lake na kuomba.
Kusudi kuu la kufunga na kuomba ni kumtafuta Mungu mwenyewe.
Yesu anasema "Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa." Mathayo 6:33
Unapofunga na kuomba, usimtafute Mungu kwa sababu tu unataka akupatie kitu; mtafute kwa sababu unamhitaji Yeye katika maisha yako.
Unapofunga, pata muda wa kukaa mbele za Mungu na kuomba. Kufunga bila maombi kunakuwa tu umeacha chakula. Wakati wa kufunga, tenga muda maalumu wa kuomba na kuwa karibu na Mungu. Mwambie Mungu mambo yaliyo moyoni mwako, msifu, mshukuru, tubu dhambi zako na mwombe akuongoze.
Luka 5:16 inasema Yesu alikuwa akijitenga kwenda mahali pasipo na watu na kuomba.
Kama Yesu alitenga muda wa kuomba, sisi pia tunahitaji kujifunza kutenga muda wa kuwa peke yetu na Mungu.
Pia ukiwa kwenye kufunga, pata muda wa kusoma neno lake. Usitumie muda wote wa kufunga ukiomba tu. Soma Neno la Mungu.
Mungu huzungumza nasi kupitia Neno lake (Zaburi 119:105). Unapofunga, soma Biblia kwa utulivu, tafakari unachosoma na mwombe Roho Mtakatifu akusaidie kuelewa kile Mungu anachotaka kukufundisha.
Reference Scriptures
Yeremia 29:13
Mathayo 6:33
Zaburi 119:105