JINSI YA KUOMBEA MWILI WAKO
Rudi kwenye Makala
Mafundisho
Innocent Morris
Kumtafuta Mungu
Baraka
Mafundisho ya Biblia
Holy Spirit Connect

JINSI YA KUOMBEA MWILI WAKO

Innocent MorrisDraft2 min read

Nimekuwa nikipata msukumo mkubwa sana kufundisha hapa hili somo lakini leo imenibidinifundishe kwa kifupi sana ili upate kitu kitakacho kusaidia usikae gizani.

Mwili kwa asili una tabia zake. Na tabia za mwili ni "Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyohaya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina,faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu." Wagalatia 5 :19-21

Kwa hiyo mwili na Roho vinapingana. "Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka." Wagalatia 5 :17

Sasa Mungu anatuasa kwamba, "kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima." 1 Wathesalonike 4 :4

Hatuwezi kujua jinsi ya kuuweza mwili bila Mungu mwenyewe kutufundisha. Kwa hiyo tunahitaji tumuombe Mungu atufundishe jinsi ya kuuweza mwili.

MAOMBI:- .

Yesu Kristo, nifundishe nijue jinsi ya kuuweza mwili wangu katika utakatifu na heshima. Amen